Saturday, 21 January 2017

Watu 3 huhitaji viungo bandia kila siku MOI.

TAASISI ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), imesema katika idadi yote ya majeruhi wanaowapokea, kila watu 50 wanaofika kunakuwepo na moja ambaye anakuwa ameumia zaidi mguu ama mkono ambao mwishowe inabidi uondolewe.

Changamoto hiyo inatokana na ukweli halisi kuwa kwa siku za hivi karibuni kila siku mtu mmoja, wawili na wakati mwingine watatu hufika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kuhitaji viungo bandia.
Sababu ya kiungo kukatwa Mkurugenzi wa Tiba MOI Dk. Samuel Swai alisema kama viungo vinakuwa vimeharibika sana husababisha hatari katika maisha ya mhusika na hivyo ni muhimu kukiondoa.
Alisema hayo wakati akifafanua taarifa yake kwamba katika idadi yote ya majeruhi wanaowapokea, kila watu 50 wanaofika kunakuwepo na moja ambaye anakuwa ameumia zaidi mguu ama mkono ambao mwishowe inabidi uondolewe.
Madai ya bodaboda kukatwa makusudi Alitoa angalizo kuwa kuna dhana potofu iliyojengeka katika jamii kuhusu taasisi hiyo kuwa, wale walioumia na pikipiki wanapofika katika taasisi hiyo wanakatwa mguu hivyo alikanusha hilo na kusema si kweli kwani uamuzi wa kumkata mguu ama mkono mtu yeyote unafanywa na jopo la madaktari wanaokaa na kuona kiungo hicho hakiwezi kutumika tena.

0 comments:

Post a Comment