Tanzania imeadhimisha Siku ya
Ukoma Duniani tar 28 1 2017 ambapo mikoa ya Lindi, Morogoro, Dar es Salaam,
Tanga na Mtwara imetajwa kuwa miongoni mwa mikoa 11 yenye idadi kubwa ya
wagonjwa wa ukoma.
Taarifa iliyotolewa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu, imezitaja
halmashauri za wilaya zinazoongoza katika mikoa hiyo kuwa ni Lindi (Lindi
Manispaa, Liwale, Lindi na Ruangwa), Morogoro (Halmashauri ya Ulanga, Kilombero
na Mvomero), Dar es Salaam (Manispaa ya Temeke na Kigamboni), Tanga (
Halmashauri za Muheza, Mkinga na Pangani).
Nyingine ni Mtwara (Halmashauri
ya Nanyumbu na Newala), Rukwa (Halmashauri ya Nkasi), Pwani (Halmashauri ya
Rufiji na Mkuranga), Geita (Halmashauri ya mji Geita na Halmashauri ya Chato),
Tabora (Halmashauri ya Sikonge), Mwanza (Halmashauri ya Kwimba na Misungwi), na
Ruvuma (Halmashauri ya Songea na Namtumbo).
Takwimu zinatuonyesha kuwa
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa huu kutoka kiwango
cha utokomezaji cha watu 0.9 kati ya watu 10,000 mwaka 2006 na kufikia
kiwango cha watu 0.4 kati ya watu 10,000 mwaka 2015 wakati kiwango cha kimataifa
cha utokomezaji ukoma kinatakiwa kuwa chini ya mgonjwa 1 katika watu
10,000.
0 comments:
Post a Comment