Monday, 30 January 2017

KUTANA NA MFUNGWA ALIYEFAULU SHULE GEREZANI NA SASA ATAKWENDA CHUO KIKUU LONDON..

Inatokea kwenye gereza la Naivasha Kenya ambapo Mfungwa Michael Kahiga ni miongoni mwa Wafungwa wachache watakaojiunga na chuo kikuu kutokana na jitihada zake za kujisomea kwa bidii chini ya Mwalimu wake pia ambaye pia ni Mfungwa wa kifungo cha maisha.

Kwenye gereza hilo la Naivasha kuna Liblary ambayo ina vitabu mbalimbali ambapo Michael anasema pamoja na yeye kufaulu kwenda chuo kikuu, kwenye kusoma kwake akiwa gerezani bado hakuwa na Waalimu ambao wamekidhi vigezo.
Michael anatumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya wizi ambapo baada ya kumaliza kifungo chake, atajiunga na chuo kikuu cha London Uingereza ambacho kimempa nafasi ya kusoma bure kwenye chuo hicho baada ya kufaulu vizuri kwenye mtihani wa kitaifa gerezani.

Kwa mujibu wa K 24 Kenya, kwenye mtihani aliofaulu Michael ni Wanafunzi 141 walipata A ambapo Michael mwenyewe alipata C+, unaweza kumtazama kwenye hii video hapa chini


Related Posts:

  • WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI….. Waalimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu… Read More
  • WATOTO WAZUIWA KWENDA SHULE KUHOFIA KUPATA MIMBA Kutokana na tatizo la upungufu wa walimu katika Shule ya Msingi Mbalawala Manispaa ya Dodoma, wazazi wa watoto wanaosoma shuleni hapo wamewazuia watoto wao kwenda shule kuanzia leo hadi hapo watakapopelekewa walimu wa ku… Read More
  • UBAKAJI WAITAFUNA UNGUJA.. Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, inakabiliwa na kasi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsi, ikiwemo matukio ya ubakaji na mimba kwa wanafunzi. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi, wa… Read More
  • WANAFUNZI KUFUNZWA KUHUSU NJIA ZA KUTOA TALAKA INDIA… Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu. Shule ya Dargh-E-Ala Hazrat inayodhibiti madrassa 15,000 za Kiislamu ilitangaza hilo kufuatia agizo… Read More
  • NECTA YAZIDI KUWABANA WALIOGHUSHI VYETI Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine. Tangazo hi… Read More

0 comments:

Post a Comment