Mwanasheria Mkuu wa Chadema
Tundu Lissu, amesema kuwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge na kata 20
si kielelezo cha Ukawa kushindwa katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.
Lissu amesema kuwa kushindwa
katika uchaguzi huo kunatokana na udogo au uchache wa maeneo yanayogombaniwa
ambayo yanawapa fursa CCM kutumia nguvu kubwa za rasilimali za kidola
ikilinganishwa na upinzani.
Amesema matokeo ya juzi si ya
kushangaza kwani kata ya Duru ilikuwa ya kwao na wameitetea, zingine zote
zilizopigwa zilikuwa za CCM.
“Hatujanyang’anywa iliyokuwa yetu tumeichukuwa,hatujanyakua
zilizokuwa za kwao,hata hivyo funzo kubwa zaidi ya chaguzi hizi ni kwamba licha
ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo hizi,tumeendelea kufanya vizuri zaidi katika
Uchaguzi Mkuu uliofuatia kipigo cha chaguzi hizi ndogo,tutumie mafundisho haya
kujipanga vizuri zaidi kwaajili ya 2020,”amesema Lissu.
Chaguzi hizo ndogo za marudio zilimalizika juzi huku CCM
ikijinyakulia kata 19 kati ya ishirini zilizokuwa zikigombaniwa Tanzania bara
na Chadema kuambulia kata moja ya Duru.
Hata hivyo Lissu amesema kuwa wapinzani hawatakiwi kunyosheana
vidole kwa kushindwa chaguzi hizo ndogo, bali wanatakiwa kurekebisha makosa na
kasoro walizoziona katika uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment