Saturday, 21 January 2017

Jammeh asema ataondoka madarakani....

.....
Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.

Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya hata tone moja la damu kumwagika.
Taangazo hilo linakuja saa kadha baada ya mazungumzo kati ya bwana Jammeh na wapatanishi wa Afrika Magharibi. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yayoafikiwa.
Bwana Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow tayari amesha apishwa.
Bwana Barrow amekuwa akiishi katika taifa jirani la Senegal kwa siku kadha.
Wanajeshi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika ikiwemo Senegal wametumwa nchini Gambia wakitisha kumtimua bwana Jammeh madarakani.
Uamuzi wa bwana Jammeh kuondoka ulikuja kufuatia mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania.

Related Posts:

  • SARAFU ZA KIRUMI ZAPATIKANA UHISPANIA..!! Katika hali ya kushangaza wafanyikazi wa ujenzi kusini mwa Uhispania, wamegundua akiba kubwa ya sarafu za kale za Kirumi nchini humo. Wafanyakazi hao wamegundua sarafu hizo,wakati wakifanya ukarabati kwenye mabomba ya m… Read More
  • MTOTO WA MIAKA 2 AMUUA MAMAKE KWA BUNDUKI..!! Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa, katika mji wa Milwaukee nchini Marekani. Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari. Mwanamke huyo Patrice Price 26 alikuwa akie… Read More
  • ASHINDA TUZO AKIWA MAHABUSU…..!! Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THDRC), umempa tuzo ya mwaka George Mgoba aliye mahabusu akikabiliwa na shtaka la kuandaa kinyume cha sheria maandamano ya vijana, waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga T… Read More
  • BALOZI WA SAUDI ARABIA AMEPEWA SAA 48 KUONDOKA ROMANIA… Balozi wa Saudi Arabia nchini Romania ambaye anakabiliwa na tuhuma ya kumbaka na kumuua sekretari wake, amepewa masaa 48 afungashe virago na kuondoka nchini humo. Mtandao mmoja wa Habari nchini humo umeripoti kwamba, … Read More
  • COLOMBIA YAHALALISHA NDOA ZA JINSIA MOJA…! Mahakama ya juu zaidi nchini Colombia, imehalalisha rasmi ndoa za wapenzi wa jinsia moja nchini humo. Hatua hiyo inaifanya Colombia kuwa taifa la nne kuhalalisha ndoa hizo katika mataifa ya Kilatino, Amerika Kusini. … Read More

0 comments:

Post a Comment