Toka ukiwa mdogo mpaka unazeeka umekuwa ukijiuliza
kwanini kila kitu unachokula au kukionja huwa kinakuwa na ladha mbaya mara tu
baada ya kusafisha kinywa chako kwa kutumia mswaki ulioweka dawa ya meno.
Dawa nyingi za mswaki huwa
zinakemikali zifuatazo Sodium lauryl sulfate, sodium laureth sulfate (SLS) and
sodium lauryl ether sulfate (SLES) ambazo hupunguza nguvu ya ukinzani ili
kutengeneza povu (foaming action) kwenye dawa ya meno ili kusaidia katika
kuondoa mabaki ya vyakula kwenye kinywa chako.
Lakini pia kemikali hizi hukinzana na utendaji kazi wa taste
buds (huhusika na utambuzi wa ladha) kwa kuvunja vunja phospholipids kwenye
ulimi wako.
Matokeo yake husababisha
ladha ya uchachu (bitter tastes) nahii ndo sababu kila unachokionja na kukila
huonekana kibaya mara baada ya kusafisha meno yako.
Lakini hali hii huondoka mara tu baada ya mda mfupi. Niwatoe
hofu watumiaji wa dawa za meno kuwa hali hii ya kuhisi uchachu haina madhara
yeyote kiafya.
0 comments:
Post a Comment