Vijisumu (antibiotics) ni mojawapo ya dawa muhimu zinazotumika mara kwa mara katika kutibu magonjwa mbalimbali yatokanayo na vimelea.
Dawa hizi hutibu magonjwa
kwa ama kuua bacteria au kupunguza uwezo wake wa kuzaliana. Ingawaje vijisumu
ni muhimu katika matibabu ya magonjwa mbali mbali kama zikitumiwa ipasavyo,
lakini matumizi mabaya huleta madhara kwa mtumiaji.
Mfano wa dawa hizi ni
ampicillin, ciprofloxacin, tetracycline, gentamycin, Pen V, erythromycin,
metronidazole, Amoxillin.
Moja ya changamoto kubwa katika matibabu ni pale baadhi ya
bacteria wanapojenga usugu dhidi ya dawa hizi. Kijiuasumu kikitumiwa kwa mda
mrefu baadhi ya bacteria hujenga usugu ya dawa hizo hivyo na hivyo kutokuwawa
na kijisuasumu hicho, hii ndiyo inayojulikana kama usugu dhidi ya vijiuasumu.
Kwa sasa magonjwa yanayosababishwa na bacteria ambao ni sugu kwa baadhi ya
vijiuasumu.
Ugonjwa unaotokana na bacteria hawa unakuwa mgumu kutibika na
unaweza kuambukizwa kwa watu wengine. Ili kutibu ugonjwa unaotokana na bacteria
hawa sugu unahitaji dawa yenye nguvu zaidi na uangalizi wa hali ya juu.
Kutumia vijiuasumu kiholela huweza kusababisha usugu wa bacteria
na hivyo kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Matumizi mabaya ya vijiua sumu ni
mojawapo ya sababu zinazoleta usugu huo. Epuka matumizi yasiyosahihi ya
vijiuasumu.
Mifano ya matumizi yasiyosahihi ya vijiua sumu:
• Kutotumia dozi kamili ya vijiuasumu na kwa muda uliolekezwa.
• Kutumia vijiuasumu kutibu magonjwa yasiyohitaji vijiuasumu kwa
mfano ugonjwa kama mafua ambao husababishwa na virusi au aleji.
• Kutumia dawa zinazokinzana kiutendaji kwa pamoja, kwa mfano
baadhi ya vijiuasumu na vidonge vya uzazi wa mpango.
• Kunywa pombe wakati ukiwa kwenye dozi ya dawa ambapo
ulishauliwa usinywe pombe.
• Kununua kiholela na kutumia dawa bila kufanyiwa uchunguzi.
• Kutumia dozi isiyo sahihi.
Ili kuepuka au kupunguza kutokea na usugu wa bacteria
unashauriwa kutumia dawa zako kwa usahihi:
• Usinunue vijisumu bila cheti cha daktari.
• Usinunue kijisumu kiholela.
• Usitumie cheti cha dawa alichoandikiwa mtu mwingine.
• Usimpe mgonjwa mwingine dawa zako.
• Usikatishe dozi unapojisikia nafuu.
• Hakikisha unafahamu matumizi sahihi ya dawa ulizopewa kabla ya kurudi
nyumbani.
• Tumia dozi sahihi kipindi chote cha matibabu.
0 comments:
Post a Comment