|
Simu iliokuwa ikitumiwa na kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler kupigwa mnada Marekan
Simu iliyokuwa ikitumiwa na Adolf
Hitler wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia itapigwa mnada nchini Marekani
mwisho mwa juma hili.
Simu hiyo nyekundu iliyo na chapa cha jina la kiongozi huyo wa
Wanazi, ilipatikana katika ngome ya Hitler jijini Berlin mwaka 1945.
Wanajeshi wa Urusi walimpa mwanajeshi wa Uingereza, Brigedia Sir
Ralph Rayner, kama kito cha kumbukumbu, muda mfupi baada ya Ujerumani kukubali
kushindwa katika vita hivyo.
|
Kampuni hiyo ya mnada iliyoko Maryland, ilisema kuwa shughuli
za mnada zitaanza kwa bei ya Dola 100,000.
0 comments:
Post a Comment