India imeweka
rekodi mpya kwa kuwa taifa lililorusha setilaiti nyingi angani kwa wakati mmoja
baada ya kurusha setilaiti 104 kwa pamoja.
Rekodi ya awali iliwekwa na Urusi mwaka 2014, ambayo ilikuwa
setilaiti 37.
Kati ya setilaiti hizo zilizorushwa India, ni tatu pekee
ambazo ni za taifa hilo huku nyingi ziiwa ni za Marekani.
Setilaiti hizo zilirushwa kutoka kituo cha safari za anga za
juu cha Sriharikota katika eneo la Andhra Pradesh mashariki mwa India.
Wachanganuzi
wanasema ufanisi huo ni ishara kwamba, India imeanza kuibuka kuwa mhusika mkuu
katika sekta ya safari za anga za juu yenye thamani ya mabilioni ya dola.
Kati ya setilaiti 104 zilizorushwa kutoka India, 96 ni za
Marekani na hizo nyingine ni za kutoka mataifa mengine yakiwemo Israel,
Kazakhstan, Umoja wa Milki za Kiarabu, Uswizi na Uholanzi.
Setilaiti ya ramani ya India ambao inaaminika kuwa na uwezo
wa kupicha picha za ubora wa hali ya juu sana kutoka angani, ni miongoni mwa setilaiti
zilizorushwa angani.
Setilaiti hiyo inatarajiwa kutumiwa na India kufuatilia
shughuli za washindani wake katika bara la Asia, Pakistan na China.
Serikali
ya India iliongeza bajeti yake kwa mpango wake wa anga za juu mwaka huu, na pia
ikatangaza mpango wa kutuma chombo sayari ya Zuhura (Venus).
0 comments:
Post a Comment