Serikali imeombwa kupiga
marufuku pombe kali zinazohifadhiwa kwenye karatasi maarufu kama ‘viroba’ ili
kuwanusuru vijana wengi wanaoathirika na kujiingiza katika ulevi wa pombe hizo.
Mkurugenzi wa kituo cha
wagonjwa na wasiojiweza cha Bashay wilayani Mbulu mkoani Manyara, Padri James
Amnaay ametoa wito huo Jumatano hii alipokabidhiwa msaada wa vyakula, nguo na
sabuni na UWT, Mbulu katika maadhimisho ya miaka 40 ya CCM.
Padri Amnaay amesema endapo Serikali itapiga marufuku pombe
hizo, vijana wengi hawatajiingiza kwenye ulevi huo unawasababisha wakithiri
katika ulevi huo na kuwafanya wawe vichaa.
Amesema kutokana na urahisi
wa kubebwa na bei nafuu, pombe hizo za karatasi zimewaathiri vijana wengi
wanaokunywa na kulewa kisha kujiingiza kwenye dawa za kulevya na kuwasababishia
kuwa vichaa.
0 comments:
Post a Comment