Thursday, 2 February 2017

MWALIMU ADAIWA KUSABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI KENYA.

Polisi nchini Kenya inachunguza kifo cha mwanafunzi wa darasa la tatu ambaye anadaiwa kupoteza maisha kufuatia kupigwa fimbo na mwalimu wake ambazo zilimsababishia majeruhi mwili mwake.

Akizungumza kuhusu tukio hilo Mkuu wa Polisi wa Kieni, Michael Mbaluku alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Joy Wangare (10) ambaye ni mwanafunzi wa Shuleya Msingi Macadamia.
Mbaluku alisema kuwa kabla ya kufariki mwanafunzi huyo, bibi wa marehemu alifungua kesi ya shambulizi Polisi na siku chache baada ya majeruhi kupatiwa matibabu alipoteza maisha hali ambayo ilizua taharuki kwa familia ya marehemu wakiamini kuwa fimbo alizochapwa mtoto wao ndiyo chanzo cha kifo.
“Bibi wa binti huyo alikuja kuripoti kesi ya shambulio dhidi ya mwalimu na tulimpa kibali ampeleke akapatiwe matibabu. Taarifa ambayo tulipokea siku chache kabla hajafariki alikwenda katika Hospitali ya Mary Immaculate na kupatiwa matibabu,” alisema Mbaluku na kuongeza.

“Hatuwezi kumshikilia muuaji kwasasa sababu ya mazingira ya kifo jinsi yalivyo tunasubiri taratibu za kisheria zikamilike, tumewataka wawe na subira na wasubiri matokeo ya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na ripoti ya uchunguzi wa marehemu.”

0 comments:

Post a Comment