Rais wa Baraza la muungano wa Ulaya Donald Tusk ameonya kwamba maamuzi ya
kutia wasiwasi yanayofanywa na Donad Trump ni miongoni mwa chanagmoto
zinazokumba muungano huo.
Amesema kuwa
mabadiliko yaliofanyika nchini Marekani ni miongoni mwa vitisho kutoka nje
vinavyojumuisha China, Urusi na Waislamu wenye itikadi kali kwa muungano huo.
Katika barua kwa
viongozi 27 wa bara Ulaya bw Tusk pia amesema kuwa anaamini kwamba wote wanakubaliana
naye.
Taarifa kadhaa kutoka
Washington zimesababisha maandamano dhidi ya Trump katika miji mikuu ya Ulaya.
Katika barua
iliotolewa kabla ya kikao cha muungano huo huko Malta wiki hii, Bw Tusk alisema
kuwa utawala mpya wa Donald Trump umeiweka EU katika hali ngumu kwa kuwa
unahoji sera ya kigeni ya Marekani ya miaka 70 iliopita.
Alimalizia kwa kusema:
Hatuwezi kusalimu amri kwa wale wanaotaka kudhoofisha ushirikiano wetu ambao
bila amani hauwezi kufanikiwa.
Tunawakumbusha
marafiki zetu wa Marekani kwamba Umoja ndio nguvu.
0 comments:
Post a Comment