Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama
kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi
mbalimbali za ukwepaji kodi.
Ameyasema hayo leo
jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa
Mahakama wenye kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa
uchumi.
Amesema kuwa
Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo
Serikali imeshinda kesi hizo japo fedha hizo hazijakusanywa mpaka
sasa.
“Kukwepa au kutolipa
kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo
ya nchi” amesema Dkt Magufuli.
Kwa upande wake Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa Mahakama imeandaa
Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani ya Mahakama.
Naye Mwanasheria Mkuu
wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba imeanisha bayana Kanuni ambazo
zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji
haki.
Siku ya Sheria nchini
ilianzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili
kuweza kusikiliza kesi.
0 comments:
Post a Comment