Mwanamke ambaye
alikuwa ametekwa nyara na wapiganaji wa Boko haram amerudi kwa wapiganaji hao
kulingana na famialia yake.
Aisha Yerima mwenye umri wa miaka 25
alizungumza na Adaobi Tricia Nwaubani kabla ya kurudi akisema:Sasa nimeona
kwamba vitu vyote ambavyo Boko haram walituambia havikuwa vya ukweli.
''Sasa nikisikiza katika redio, nacheka''.
Alitoa matamshi hayo baada ya kukamilisha mpango wa kumuondolea itikadi kali,
lakini chini ya miezi mitano baadaye aliitoroka familia yake na kurudi kwa
wapiganaji hao.
Wakati alipotekwa na wapiganaji hao alikuwa
ameolewa na kamanda ambaye alimfurahisha kwa mapenzi,na kumpa zawadi zenye
thamani mbali na kumuimbia nyimbo za mapenzi za kiarabu.
Mwanasaikolojia Fatima Akila ambaye amefanya
kazi na mamia ya wanawake waliookolewa anasema kwamba mara nyengine wanaonyesha
kuwa na uwezo mkubwa.
''Hawa ni wanawake ambao kwa kipindi kirefu
hawakuwa wakifanya kazi, hawakuwa na uwezo, hawakuwa na sauti katika jamii na
mara moja wakaanza kuwasimamia kati ya wanawake 30 jadi 100 ambao walikuwa
chini ya udhibiti wao''.
0 comments:
Post a Comment