Tuesday 18 July 2017

TUNDU LISSU ATEMA CHECHE….

Wakati Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, akiwa
bado anakabiliwa na kesi kadhaa za uchochezi, amefytuka tena na kutoa maneno mazito juu ya viongozi wa Serikali, huku akisema kwa mujibu wa sheria za nchi, anaweza kukamatwa, lakini si kufungwa.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Lissu pia alisema amepata taarifa kutoka kwa mmoja wa askari polisi kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, atafikishwa mahakamani wakati wowote kutokana na kauli alizozitoa juu ya masheikh wa Uamsho.
Akizungumzia taarifa za Lowassa kufikishwa mahakamani, alisema amezipata kutoka kwa mmoja wa maofisa wa ngazi za juu ndani ya Jeshi la Polisi.
Lissu alisema kuwa aliwasiliana na ofisa huyo jana asubuhi na kumtaka ajiandae kwa kesi hiyo ambayo ipo mbioni kupelekwa mahakamani.
 “Nina taarifa nimeambiwa leo na lipolisi likubwa kabisa, maana hata wao hawafurahi sana, nimeambiwa jiandaeni mheshimiwa Lowassa atafikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya kuzungumzia uonevu wanaofanyiwa masheikh wa Uamsho,” alisema Lissu.

Alipoulizwa endapo kinga za kushtakiwa kwa viongozi, inawahusu pia mawaziri wakuu wastaafu, alisema kinga inamuhusu rais aliyepo madarakani pekee na mambo aliyofanya wakati akiwa Ikulu.

0 comments:

Post a Comment