![]() |
Msaada wa fedha kwa wakimbizi unawawezesha kujikwamua kiuchumi |
Serikali ya Ufaransa imechangia kiasi
cha Euro 250,000 kwa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP ili wakimbizi
nchini Tanzania waweze kupata msaada zaidi wa kifedha.
Msaada
huu unadhihirisha mchango wa serikali ya Ufaransa katika kuhakikisha kuna hali
ya usalama wa chakula.
Mwezi
Desemba mwaka jana, WFP ilianza kusambaza shilingi za kitanzania 20,000 sawa na
dola 9 za marekani kila mwezi kwa wakimbizi 10,000 ukiwa ni mpango wa majaribio
uliotekelezwa kwa kushirikiana na washirika ikiwemo serikali ya Tanzania na
shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
Mchango
wa Ufaransa unaiwezesha WFP kuendeleza mradhi huu wa kutoa fedha kwa wakimbizi
10,000 kwa kipindi cha miezi miwili zaidi.
Chini
ya mradi huu, wakimbizi wanapokea mgao wa mafuta yatokanayo na mimea, unga kwa
ajili ya uji, wakati mgao wa mahindi, na chumvi hubadilishwa kwa fedha.
Kabla
ya uzinduzi wa utoaji mgao wa fedha, wakimbizi walikuwa wakipokea msaada wa
chakula pekee kutoka WFP.
Kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa hivi karibuni, asilimia 98 ya wakimbizi wanapenda zaidi
kupatiwa msaada wa fedha wakati asilimia 83 wamesema zimewasaidia katika
kuimarisha matumizi ya chakula na kupata aina mbali mbali za vyakula.
''Matokeo
ya mpango huu wa,msaada wa fedha umekua si njia pekee inayopendelewa na
wakimbizi zaidi ya msaada wa chakula lakini pia ni njia ambayo inasaidia kukuza
uchumi wao,'' amesema Michael Dunford, mwakilishi wa WFP nchini Tanzania.
Miaka
ya karibuni,shirika hilo limekua likiongeza kiasi cha msaada linalotoa kwa
mtindo wa fedha na vocha.
Asilimia
29 ya wanaonufaika na WFP hupokea msaada wa chakula kwa njia ya fedha.
Tangu
kutokee hali ya kutetereka kwa usalama nchini Burundi mwaka 2015, zaidi ya raia
250,000 wa nchi hiyo walitafuta hifadhi nchini Tanzania, ambayo sasa imewapa
makazi wakimbizi 315,000, wengi wao kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ifikapo
mwishoni mwa mwaka, WFP ina mpango wa kuongeza mgao wa fedha kwa wakimbizi
80,000, shirika linahitaji dola za marekani milioni 6.8 kwa mwezi kuendelea na
mpango wa kutoa fedha na chakula kwa wakimbizi nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment