Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku
urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila
kupata kibali maalum.
Kupitia tangazo lake kwa umma, TCAA imesema kuwa kwa taasisi au
mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya
Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.
“Ifahamike kuwa kuanzia sasa, taasisi au mtu binafsi anayetaka
kununua, kufanya majaribio au kurusha angani vifaa hivyo visivyotumia rubani
anapaswa kupata idhidi ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na kibali kutoka
TCAA,” imeeleza taarifa ya Mamlaka hiyo.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza
Johari imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya
Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Tangazo hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na urushwaji wa
drones unaofanywa na watayarishaji wa video za muziki kwa lengo la kuchukua
picha za juu, pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua matukio husika hasa
yanapofanyika katika maeneo ya wazi.
Drones zilitumika zaidi katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo
mikutano ya kampeni za wanasiasa ilikuwa ikipigwa picha za juu kuonesha umati
uliohudhuria.
0 comments:
Post a Comment