Friday, 7 July 2017

MWANAMKE AIKOJOLEA BENDERA YA MAREKANI...

Mwanamke aliyesambaza kanda yake ya video akiikojolea bendera ya Marekani ametoa wito kwa watu kutoilenga familia yake akisema hawaungi mkono tendo lake.

Emily Lance alipokea vitisho vya mauaji katika mtandao wa kijamii na ubakaji baada ya kuchapisha kanda hiyo ya video siku ya uhuru wa taifa hilo.
Akaunti yake haiko tena katika mtandao wake wa facebook lakini awali alikuwa amechapisha kwamba babake na eneo analofanya kazi pia limelengwa, kulingana na ripoti.
Kutoheshimu bendera ya Marekani sio kinyume cha sheria kutokana na sheria nyingi na uhuru wa kujieleza.
Katika kanda hiyo ya video, Bi Lance anaonekana akisimama juu ya choo ambapo bendera ya Marekani imewekwa na kuikojolea kupitia usaidizi wa chombo ambacho kinawasaidai wanawake kufanya hivyo wakiwa wamesimama.
Chini yake aliandika maneneo ya kuitusi bendera hiyo.

Baadaye aliwataka wanaopinga wazo lake kutowalenga watu wasio na hatia akisema hakuna hata mtu mmoja katika familia yake anayeunga mkono wazo lake.

Related Posts:

  • MAREKANI YASEMA KOREA YA KASKAZINI NI TATIZO.. Rais wa Marekani, Donald Trump ameizungumzia Korea ya Kaskazini baada ya kitendo chake cha hivi karibuni cha kurusha kombora lenye uwezo wa kubeba silaha za kinyuklia kwamba nchi hiyo ni hatari kwa usalama wa dunia. Tru… Read More
  • ALIYETEULIWA NA TRUMP KUWA WAZIRI AJITOA.. Andrew Puzder aliyekuwa ameteuliwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa waziri wa masuala ya wafanyakazi, amejiondoa muda mfupi kabla ya kuhojiwa na wabunge. Puzder alipoteza uungwaji mkono wa maseneta kadha wa cham… Read More
  • WALIOONGOZA MGOMO WA MADAKTARI WAACHIWA HURU Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imeamuru kuachiliwa huru mara moja kwa viongozi wa chama cha wauguzi na madaktari nchini humo waliohukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela. Viongozi hao saba walifungwa Jumatatu wiki … Read More
  • AMUUA MFANYAKAZI AKIDHANI NI NGIRI AFRIKA KUSINI.. Watu nchini Afrika Kusini wamegadhabishwa, kufuatia taarifa za mwanamme mmoja, ambaye analaumiwa kwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyakazi wa shamba, akidhani kuwa mtu huyo ni ngiri. Stephen Hepburn alifikishwa mahakaman… Read More
  • SIMU YA ADOLF HITLER KUPIGWA MNADA MAREKANI. Simu iliokuwa ikitumiwa na kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler kupigwa mnada Marekan Simu iliyokuwa ikitumiwa na Adolf Hitler wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia itapigwa mnada nchini Marekani mwisho mwa juma hili. Simu… Read More

0 comments:

Post a Comment