Wednesday, 12 July 2017

UTAFITI WABAINI RUSHWA KUPUNGUA KWA KASI NCHINI……

Jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli za kupambana na rushwa, zimewafanya wananchi kuamini kuwa hivi sasa vitendo hivyo vinapungua kulinganisha na miaka
iliyopita.
Hayo yamebainika kutokana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM, kupitia Idara ya Sosholojia kwa kushirikiana na taasisi inayojishughulisha na masuala ya utawala ya Basel Switzerland.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua utafiti huo uliofanywa mwaka jana katika mikoa ya Dar es Salaam na Kagera, Mtafiti Msaidizi wa UDSM Egidius Kamanyi amesema kuwa, katika kipindi cha nyuma tatizo la rushwa lilikuwa linachukuliwa kawaida katika jamii tofauti na ilivyo sasa.
Amesema katika utafiti huo wamebaini kwamba kwa sasa jamii inaogopa kwa kiasi kikubwa kujihusisha na rushwa kuanzia katika huduma ndogo ndogo hadi kubwa.

Amesema katika utafiti huo wamebaini kwa sasa kila mmoja anaogopa kujihusisha nayo na kwamba huduma nyingi zinapatikana kwa urahisi pasipo usumbufu tofauti na ilivyokuwa nyuma hususani katika sekta ya afya.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment