Bohari ya Dawa (MSD) imetangaza kubadilisha vifungashio vya dawa kutoka kwenye
vifungashio vya
makopo kwenda kwenye vifungashio vilivyo kwenye mfumo wa
blister Pack ili kuzifanya dawa ziwe salama zaidi kulingana na maelekezo ya
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alisema mwishoni
mwa wiki kuwa, kwa muda mrefu MSD ilikuwa ikiuza dawa ambazo ziko kwenye
vifungashio vya makopo ambapo watoa huduma huwapimia wagonjwa kiasi cha dawa
wanachokihitaji na kisha kuwawekea kwenye vifungashio vya dawa.
“Kuanzia mwaka huu wa fedha MSD imeanza kuagiza dawa
kutoka kwa wazalishaji zikiwa zimefungwa kwenye mfumo wa blister pack, dawa
hizo sasa zitamwezesha mtumiaji kuzitunza kwa hali ya usafi na usalama zaidi
kwa mujibu wa miongozo ya utunzaji dawa,” alisema Bwanakunu.
Vifungashio vya makopo vilikuwa na changamoto kadhaa na huko
nyuma, TFDA iliwahi kubaini dawa za kupunguza makali ya ukimwi zikiwa zimewekwa
kwenye vifungashio vya makopo vya dawa huku makopo hayo yakiwa tofauti na
vifungashio vya dawa vilivyosajiliwa na TFDA.
0 comments:
Post a Comment