Thursday, 6 July 2017

UGANDA YAPIGA MARUFUKU WANAWAKE KUVAA SKETI FUPI KAZINI….

Serikali nchini Uganda imewapiga marufuku wanawake wanaofanya kazi katika ofisi za Umma kuvaa nguo fupi na zile zinaoonesha miili yao.

Wafanyikazi hao wameambiwa kuwa ni marufuku uvaa mawazi yanaonesha mapaja, sehemu ya matiti yao.
Agizo hili si tu kwa wanawake,wanaume pia wametakiwa kuvaa nguo za mikono mirefu, tai na kutovaa suruali za kushuka.
Pamoja na hilo, wanaume wametakiwa kukata kucha na nywele zao kuwa fupi lakini pia kuepuka kuvaa nguo zinazo ng'aa.
Wizara ya Utumishi wa Umma imesema wafanyikazi watakaokwenda kinyume na masharti haya watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Aidha Wizara hiyo imesema wanawake wanaweza kuvaa suruali lakini isiwe ya kubana lakini pia sketi isiwe fupi.

Ripoti zinasema kuwa kanuni hizi zimekuwepo tangu mwaka 2010 lakini zimekuwa hazitekelezwi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment