Monday 10 July 2017

MARUFUKU YA LAPTOP YAONDOLEWA MASHIRIKA 2 YA NDEGE…

Mashirika mawili ya ndege ya Kuwait Airways na Royal Jordanian, yameruhusiwa kuruhusu abiria wake kubebea laptop ndani ya ndege zinazoelekea Marekani.

Mashirika hayo mawili yamesema yameshirikiana na maafisa wa Marekani kuimarisha usalama kwa ndege zinazotoka nchini Kuwait na Jordan.
Marekani ilitangaza marufuku hiyo mwezi Machi kwa safari za moja kwa moja kutoka nchi nane za kiislamu, kutokana na hofu kuwa mabomu yangebebwa ndani ya vifaa hivyo.
Mashirika ya ndege ya Etihad, Turkish Airlines, Emirates na Qatar yaliondolewa marufuku hiyo wiki iliyopita.
Shirika la Royal Jordanian ambalo hufanya safari katika miji mitatu ya Marekani kutoka Amman mji mkuu wa Jordan, liliondoa marufuku hiyo baada ya hatua mpya za kiusalama zilizochukuliwa kwenye ndege zinazoelekea nchini Marekani.

Shirika linalomikiw na serikali la Kuwait Airlines ambalo hufanya safari zake kutoka Kuwait kuenda mjini New York likipitia Ireland, limesema marufuku hiyo ilitolewa baada ya maafisa wa Mareknian, kukagua usalama kwenye safari zake.

0 comments:

Post a Comment