Wednesday 12 July 2017

MZEE MWENYE WATOTO 100 ANASEMA ANA NIA YA KUONGEZA ZAIDI….

Wakati ulimwengu ulipoadhimisha siku ya idadia ya watu duniani mwanamume mmoja alikuwa na sababu 100 za kusherehekea.

Kofi Asilenu mwenye umri wa miaka 80 ni baba wa watoto 100 na wake 12.
Anaishi na familia yake katika kijiji cha Amankrom kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu Acca.
Familia yake ni thuluthi moja ya watu 600 katika kijiji hicho.
Anasema kuwa anataka familia kubwa kwa sababu hakuwa na ndugu.
Amesema hana kaka wala shangazi,ndio sababu aliamua kuwa na watoto wengi ndio wapate kumpa maziko yaliyo mazuri siku akifariki.
Ameongeza kuwa familia hiyo imemgharimu pakubwa,kwani alikuwa mtu mwenye mali nyingi, lakini male hiyo ilipungua kutokana na gharama ya kuitunza familia yake kubwa

Kofi Asilenu anaonekama kuwa mwenye afya nzuri na hata anasema kuwa anataka kuwa na watoto zaidi.

0 comments:

Post a Comment