Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka kampuni za
simu za mikononi nchini, kusitisha matangazo wakati wateja wanapiga simu
vinginevyo wataadhibiwa.
Akizungumza jijini hapa leo Alhamisi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA
Mhandisi James Kulaba, amesema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja
kuwa wanapopiga simu huanza kusikiliza matangazo ya kampuni hizo badala ya watu
wanaowapigia.
Amesema sheria na kanuni za kumlinda mtumiaji wa huduma za
mwaka 2011 zinataka watoa huduma kutoa matangazo wakati wa kumjibu mteja
anapoulizia salio la muda wa maongezi.
Kulaba amesema watoa huduma wanaweza kutangaza wakati mteja
anapopokea taarifa baada ya kuongeza salio na anapoingia katika orodha ya
huduma za kampuni husika.
Kulaba amesema wateja wameonyesha hisia ya kukerwa na
utitiri wa matangazo yasiyozingatia kanuni za mamlaka hiyo.
Kuhusu adhabu Kilaba amesema kuna aina nyingi za adhabu
zinazoweza kutolewa ikiwemo kuzifungia kabisa zisifanye kazi nchini
0 comments:
Post a Comment