Monday, 24 July 2017

ADAKWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI MAABARA..

Mwalimu wa somo la Baiolojia katika shule ya sekondari ya wasichana ya St Therese mjini Lusaka ambaye alidakwa akifanya mapenzi na mwanafunzi katika maabara ya shule hiyo amesimamishwa kazi akisubiri hatua za kinidhamu dhidi yake.

Ofisa Elimu wa Wilaya, Christopher Sinkamba akizungumza alisema kwamba maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya wananchi wengi kulalamika.
Sinkamba alisema mwalimu anayehusika ametambuliwa kama Raphael Mwape na kwamba sasa anasubiri hatua za kinidhamu dhidi yake.
Alisema kwamba utawala wa shule ulifikisha suala hilo Polisi lakini walishindwa kumshtaki kwa tuhuma za kubaka kwa kuwa binti huyo ni zaidi ya miaka 16.
Na wakati alipoulizwa swali kwanini mwanafunzi huyo wa kike ametimuliwa shule, ofisa huyo alisema kwamba hawajamfukuza lakini walilazimika kumhamisha shule kutokana na sheria za shule hiyo.
Ilielezwa kuwa tukio hilo lilifanyika saa 12 jioni ambapo Mwape alionwa na mabinti wengine wawili wa shule hiyo akifanya mapenzi na binti huyo katika maabara B ya shule hiyo. Mwanafunzi huyo alisema kwamba hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mwalimu huyo kumuingilia na kwamba siku hiyo alilazimika kufanya hivyo baada ya kushinikizwa na mwalimu aliyemuita wakati akirejea bwenini.

Alisema pamoja na kukataa kwake alimshinikiza kwa kudai kuwa alikuwa amemgharamia sana.Mwalimu huyo ana mke.

Related Posts:

  • POLISI WAKAMATA WANACHAMA WA DHEHEBU HARAMU CHINA... Polisi nchini China wamewakamata wanachama 18 wa dhehebu lililopigwa marufukua. Baadhi ya wanachama wa kundi hilo ni maarufu kwa kumpiga mwanamke hadi kufa kwenye duka la McDonald mwaka 2014, baada ya mwanamke huyo ku… Read More
  • MKUU MPYA WA FBI APATIKANA…… Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kuthibitishwa Bwana Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI. Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipotimuliwa na Rais Dona… Read More
  • RAIS MUSEVENI: SIJAUGUWA KWA MIAKA 31 Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafan… Read More
  • MWIZI AKUTWA AMELEWA NDANI YA NYUMBA ALIOVUNJA…. Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia kwa wizi, baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani. Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na ku… Read More
  • MWANAFUNZI AKAMATWA KWA KUMKASHIFU RAIS KWENYE FACEBOOK.... Jeshi la polisi nchini Zambia linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, kwa tuhuma za kumkashifu Rais Edgar Lungu na maafisa wengine wa Serikali kwenye Facebook. Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Esther… Read More

0 comments:

Post a Comment