Monday 17 July 2017

WAUMINI WAWILI WAFA MAJI WAKIBATIZWA..

Waumini wawili wa Kanisa Siloam wamekufa maji wakibatizwa katika Mto Ungwasi wilayani Rombo baada ya mmoja wao kupandisha mapepo na kuwatumbukiza majini wenzake.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro Agnes Hokororo, amethibitisha tukio hilo lililotokea jana saa sita mchana.
Ubatizo huo ulifanyika kwenye kina kirefu cha mto huo.
Amesema wakati ibada ya ubatizo mmoja wa waumini aliyepandisha mapepo alimtumbukiza mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri kubatizwa na mchungaji.
Hokororo amesema muumini mmoja alipoona mwenzake ametumbukizwa majini aliamua kumwokoa, ndipo aliyepandisha pepo alipowashikilia wote wawili ndani ya maji na kuwasababishia kifo.

Amesema watu watatu akiwamo mchungaji wa kanisa hilo lililopo katika Kijiji cha Mandechini wanashikiliwa.

0 comments:

Post a Comment