Kisiwa
cha Cook ndio bingwa duniani wa shindano la ukweaji minazi imeripotiwa.
George
Iona aliibuka mshindi katika shindano lillilokuwa na wawaniaji 16,akishinda kwa
uchache kulingana na idhaa ya redio ya Tahiti.
Aliupanda
mti huo wenye urefu wa mita nane kwa sekunde 5.62 katika shindano hilo
lililofanyika katika eneo la kumbukumbu la Tahiti.
Alikuwa
mbele ya Fiapai Ellio wa Samoa ya Marekani mtu aliyepigiwa upato kushinda.
Lengo
la shindano hilo jipya ,ni kupanda mti huo haraka iwezekanavyo huku kila
mpandaji akipewa fursa mbili za kuweka muda bora zaidi.
Hatua
hiyo inashirikisha kuvaa kamba katika visigino vya miguu ili kusaidia kukwea
kwa garaka.
Akizungumza
na idhaa ya redio ya Tahiti 1, mwaandalizi Enoch Laughlin amesema kuwa ushindi
mkubwa wa bwana Iona uliwashangaza watu wengi, kwa kuwa kila mtu alitarajia
kwamba mwanariadha wa Samoa ataibuka mshindi kufuatia ushindi wao katika
mashindano ya awali.
Mshindi
huyo aliwaambia maripota kwamba ni fahari kubwa na furaha kushinda taji hilo.
0 comments:
Post a Comment