Thursday, 6 July 2017

BAVICHA WATOA NENO KWA WATEULE WA JPM…

Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limetoa wito kwa wateule wa JPM wakuu wa mikoa wakiwemo wakuu wa Wilaya kupatiwa semina elekezi ili wajifunze mifumo na utendaji wa utumishi wa umma kwa madai kuwa wengi wao hutumia vibaya madaraka waliyopewa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa baraza hilo, Julius Mwita alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, amesema kuwa baraza hilo limefikia hatua hiyo mara baada ya viongozi wake kukamatwa mara kwa mara kwa amri ya wakuu wa Wilaya na Mikoa.
Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea, Juma Nassoro amesema kuwa Sheria ya Tawala za Mikoa namba 19 ya mwaka 1997 vifungu vya 7(9) na 15(9) vinatoa maelekezo kuwa endapo kiongozi husika atabainika kutumia vibaya madaraka yake anaweza kushtakiwa chini ya Sheria ya Makosa ya Jinai.“Kiongozi hana mamlaka ya kumweka mtu ndani kama adhabu, bali anakamatwa ili afikishwe mahakamani ndani ya saa 48, hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kumwazibu mtu mwingine isipokuwa Mahakama,”amesema Nassoro
Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la ukamatwaji wa viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee,Meya wa Ubu8ngo, Jacobo Steven, mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea na Ester Bulaya wa Bunda mjini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment