Wednesday 12 July 2017

ROONEY AITEKA DAR………

 
Mshambuliaji mpya wa Everton Wayne Rooney, amekuwa kivutio wakati msafara wa timu hiyo ulipowasili jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Everton iliyowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa (JNIA) ilipokelewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe.
Ndege binafsi ya Everton iliwasili katika uwanja huo majira ya saa 2:39 Asubuhi,kabla ya wachezaji kuanza kuingia kwenye basi lao maalumu, huku wakipitia kwa Waziri Mwakyembe na kumpa mkono.
Wakati wachezaji wa Everton wakiingia kwenye basi, mashabiki waliokuwa nyuma ya geti la kuingilia VIP kila mmoja alionyesha shauku ya kumuona mubashara 'live' Rooney ,ambaye kana kwamba msafara huo ulilitambua hilo na Rooney kuwa wa mwisho kushuka.
Aliposhuka Rooney alikwenda kumpa mkono Waziri Mwakyembe na kisha kuelekea kwenye basi maalumu la timu hiyo, wakati akielekea kwenye basi baadhi ya mashabiki wake waliokuwa uwanjani hapo walianza kupaza sauti wengine wakitaka ageuke asimame na kupunga mkono.

 Everton itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

0 comments:

Post a Comment