Monday 10 July 2017

NGELEJA ARUDISHA MGAWO WA ESCROW…

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema CCM William Ngeleja, ametangaza kurejesha pesa za Escrow.

Ngeleja amesema katika kipindi cha zaidi ya miaka 12 akiwa kiongozi wa umma, hakuwahi kukumbwa na kashfa yoyote ya rushwa na ufisadi.
Ameyasema hayo leo wakati akitangaza uamuzi wake wa kurudisha shilingi milioni 40.4 za mgawo wa Escrow, alizozipokea kutoka kwa mfanyabiashara James Rugemalira.
Ngeleja amesema amerudisha fedha hizo baada ya kusononeka na kufadhaika, kutokana na msaada huo aliopewa kuhusishwa na tuhuma.
Kuhusu kuchelewa kurudisha fedha hizo baada ya Rugemalira kutuhumiwa Ngeleja amesema kuwa, alishindwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa haikuthibitishwa kama mfanyabiashara huyo ana kashfa.

0 comments:

Post a Comment