Wednesday, 19 July 2017

AJUZA WA MIAKA 86 ASHTAKIWA KWA WIZI….

Ajuza wa miaka 86 anayejulikana sana kwa wizi wa vito tangu miaka ya 50 ameshtakiwa kwa wizi.
Doris Payne alikamatwa katika duka moja katika eneo la Chamblee mjini Georgia kwa wizi wa vito vyenye thamani ya dola 86 kulingana na maafisa wa polisi.

Ameachiliwa kwa dhamana.
Alipatikana amevalia kifaa cha kumfuatilia mtu mguuni katika shtaka jingine la wizi wa dukani.
Payne amehudumia vifungo kadhaa kwa uhalifu aliotekeleza.
Anadaiwa kuiba vito vyenye thamani ya dola milioni 2 na akaangaziwa katika makala ya 2013.
Mfanyikazi mmoja wa duka alisema kuwa aliiba vitu kadhaa kutoka kwa duka la dawa , vifaa vya kielektroniki na katika duka la mboga.
Wakili wake Drew Finding alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema: Hiki ni kisa cha kipekee ikilinganishwa na visa vyengine vilivyopita.
Tunazungumzia kile bibi wa miaka 86 anachotaka ili kuweza kuishi kila siku, ikiwemo chakula na matibabu.
Hivi karibuni alikiri kuiba mkufu kutika duka moja huko Atlanta.

Alihukumiwa kifungo cha nyumbani na kupigwa marufuku kuingia katika maduka ya jumla katika eneo hilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment