Thursday 27 July 2017

MWANAFUNZI AKAMATWA KWA KUMKASHIFU RAIS KWENYE FACEBOOK....

Jeshi la polisi nchini Zambia linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, kwa tuhuma za kumkashifu Rais Edgar Lungu na maafisa wengine wa Serikali kwenye Facebook.


Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Esther Katongo amesema kuwa, mwanafunzi huyo amedaiwa kufungua ukurasa wa Facebook kwa jina ‘feki’ na kuutumia kumkashfu Rais Lungu.

Katongo ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo pia aliutumia ukurasa huo kwa muda mrefu, kuwakashfu na kuwatukana mawaziri wa Serikali ya nchi hiyo, viongozi wa chama tawala, msemaji wa Rais Lungu na mkuu wa jeshi la polisi la Zambia.

Msemaji huyo wa jeshi la polisi amesema kuwa, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na kwamba atafikishwa mahakamani leo.

0 comments:

Post a Comment