Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO) limesema kuwa, watu milioni 20 wanasumbuliwa na njaa na utapiamlo
lote duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa FAO, José Graziano da Silva ambaye
alikuwa akihutubia mkutano wa siku sita wa jumuiya hiyo katika mji mkuu wa
Italia, Roma amesema kuwa, njaa inabidi ikomeshwe kote duniani kufikia mwaka
2030 na kuongeza kuwa, vita na mapigano yanayoongezeka katika nchi mbalimbali
ni miongoni mwa sababu za mgogoro wa njaa diniani.
Mkutano wa 40 wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO) ulioanza tarehe 3 Julai na utaendelea hadi tarehe 8 mwezi huu,
utachagua wanachama na mwenyekiti mpya wa baraza la shirika hilo.
Mkutano huo ndio kikao muhimu zaidi cha kuchukua maamuzi na
hufanyika mara mbili kwa mwaka ukishirikisha marais wa baadhi ya nchi, mawaziri
wa kilimo na maafisa wa ngazi mbalimbali wa nchi 194 wanachama wa FAO.
Mkutano wa mwaka huu unajadili hali ya
upatikanaji wa chakula, jinsi ya kusimamia ukame na uhaba wa maji, kilimo cha
familia, jinsi ya kupunguza hasara za mazao ya kilimo na kadhalika.
0 comments:
Post a Comment