Wednesday, 19 July 2017

MBUNGE ANAYEMKOSOA ZUMA KULINDWA….

Mkosoaji mashuhuri wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, atapewa ulinzi wa polisi baada ya kupokea vitisho vya kuuliwa.

Bunge na polisi walifanya uchunguzi na kubaini kuwa kuna vitisho vya kuuliwa dhidi ya Makhosi Khoza ambaye ni mbunge wa chama cha ANC.
Bi Khoza amemtaka Bwana Zuma aondoke madarakani akimtaja kuwa kiongozi wa kuchukiza ambaye amekumbwa na madai ya ufisadi.

Zuma anakana kufanya lolote baya na hakuna madai kuwa amehusishwa na vitisho hivyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment