Wednesday 26 July 2017

MAGARI YANAYOTUMIA MAFUTA KUONDOLEWA BARABARANI UINGEREZA KUANZIA 2040…..

Magari mapya yanayotumia mafuta ya diseli na petroli nchini Uingezeza yataandolewa barabarani kuanzia mwaka 2040 kama njia ya kukabiliana na uchafuzi wa hewa.

Mawaziri pia watazindua ufadhili wa paunia milioni 255 kusaidia kukabiliana na gesi chafu kutoka kwa magari yanayotumia diseli ikiwa ni sehemu ya pauni bilioni 3 za kusaidia kusafisha hewa.
Serikali baadaye itaanza mikakati yake ya hewa safi ambayo itapendelea magari yanayotumia umeme.
Wanaotetea hatua hii wanataka serikali kufadhili kuwepo sehemu zenye hewa safi huku wale walio na magari yanayochafua wakilipishwa.
Baada ya kesi mahakamani serikali iliamrishwa na mahakama kubuni mipango mipya na kutangaza viwango vipya vya uchafuzi wa hewa.
Mawaziri walilazimika kutangaza mikakati ya kusafisha hewa mwezi mei huku hatua za mwisho zikitajwa tarehe 31 mwezi huu.


Baadhi ya hatua hizo ni kuyafanyia ukarabati mabasi na mifumo mingine ya usafiri ili iwe misafi zaidi.

0 comments:

Post a Comment