Dhana
potofu kuwa unywaji kahawa unaleta shinikizo la damu, umesababisha kinywaji
hicho kutumika kwa asilimia 10 tu nchini.
Akizungumza
katika Banda la Bodi ya Kahawa Tanzania lililopo katika viwanja vya Maonyesho
ya Kimataifa ya 41 (Sabasaba), Ofisa Uhamasishaji wa bodi hiyo, Frank Mlay
amesema dhana hiyo imesababisha zao hilo likose thamani hapa nchini.
Badala
yake, Mlay amesema kinywaji cha zao hilo kina faida nyingi za kiafya ikiwa ni
pamoja na kuzuia saratani, ugonjwa wa kutetemeka (Parkinson Disease) na maumivu
ya ngozi.
Amesema
asilimia 90 ya kahawa inasafirishwa nje ya nchi na asilimia 10 pekee ndiyo
inayotumika hapa nchini.
Meneja
masoko na ubora wa bodi hiyo, Rogalus Meela amesema kama Watanzania wataitumia
kahawa ipasavyo wataiongezea mnyororo wa thamani ambapo akija mnunuzi kutoka
nje atalazimika kuinunua kwa bei ya juu.
0 comments:
Post a Comment