Monday, 17 July 2017

TELEGRAM KUFUNGA AKAUNTI ZA MAKUNDI YA UGAIDI INDONESIA…

Mtandao wa kutuma ujumbe kwa njia ya simu wa Telegram, umeahidi kuwa utafunga akaunti zinazohusiana na ugaidi, baada ya serikali ya Indonesia kufunga huduma za mtandao huo nchini humo.

Wizara ya mawasialiano na teknolojia nchini Indonesia, ilifunga huduma za Telegram siku ya Ijumaa na kutishia kufunga mifumo yake yote.
Indonesia inadai kuwa Telegram imetumiwa kuunga mkono itikadi kali na kutoa maelekezo ya kufanya mashambulizi.
Mwanzilishi wa mtandao huo amesema kuwa, ameghadhabishwa na hatua hiyo.
Katika taarifa Pavel Durov alisema kuwa, Telegram sasa imeondoa akaunti zote zinazohusika na ugaidi zilizotajwa na serikali.
Hatua ya serikali inakuja huku kukiwa na wasi wasi wa kuibuka kwa kundi la Islamic State kusini mashariki mwa Asia.

Kundi hilo limedai kuhusika kwenye mashambulizi kadha nchini Indonesia mwaka huu na limepigana na jeshi mjini Marawi katika kisiwa cha mindanao nchini Ufilipino.

Related Posts:

  • MWIZI AKUTWA AMELEWA NDANI YA NYUMBA ALIOVUNJA…. Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia kwa wizi, baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani. Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na ku… Read More
  • RAIS MUSEVENI: SIJAUGUWA KWA MIAKA 31 Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafan… Read More
  • MKUU MPYA WA FBI APATIKANA…… Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kuthibitishwa Bwana Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI. Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipotimuliwa na Rais Dona… Read More
  • BIBI HARUSI AJARIBU KUMUUA MUMEWE BAADA YA NDOA Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani, ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa. Kate Elizabeth Prich… Read More
  • KAMPUNI YA CHINA YASHTAKIWA KWA KUCHAFUA MAZINGIRA GAMBIA….. Wanamazingira kutoka miji midogo ya pwani nchini Gambia wameipeleka kampuni moja ya China mahakamani kwa madai ya kutupa takataka za sumu kwenye bahari. Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kukubaliana nje ya mahakama n… Read More

0 comments:

Post a Comment