Monday, 3 July 2017

RUGEMARILA NA BOSI WA IPTL WAONGEZEWA MASHTAKA 6….

Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engeneering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira (kushoto) na Habinder Seth Sigh (kulia) Mwenyekiti Mtendaji wa PAP.

Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engeneering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira na Habinder Seth Sigh, Mwenyekiti Mtendaji wa PAP wamefikishwa mahakamani Jumatatu hii na kuongezewa mashtaka mengine sita ya kuhujumu uchumi.

Awali watuhumiwa hao walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma ya uhujumu uchumi na kula njama, kughushi, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababisha hasara serikali, lakini watuhumiwa hao leo tena wamepandishwa kizimbani na kuongezewa makosa mengine sita ya ya utakatishaji wa fedha na kufikisha jumla ya mashtaka 12.

Mbali na hilo watuhumiwa hao wamekwama baada ya kukosa dhamana tena na wote wamerudishwa rumande mpaka tarehe 14 Juni mwaka huu ambapo kesi yao itasomwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment