Friday, 7 July 2017

BETRI KUBWA ZAIDI DUNIANI KUUNDWA..

Betri kubwa zaidi ya lithium duniani itaundwa na kuwekwa nchini Australia, kupitia makubaliano kati ya kampuni inayounda magari ya kutumia umeme ya Tesla na kampuni ya kawi ya Australia Neoen.

Betri hiyo inatarajiwa kulikinga jimbo la Australia Kusini dhidi ya mgogoro wa kawi sawa na uliosababisha kukatizwa kwa umeme kabisa katika jimbo hilo Septemba 2016 baada ya kutokea kwa tufani mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 50, waziri mkuu wa jimbo hilo Jay Weatherill.
Watu zaidi ya 1.7 milioni huishi katika jimbo hilo ambalo ni kubwa mara 40% zaidi ya jimbo la Texas. Jimbo hilo lina ukubwa wa zaidi ya kilomita mraba 980,000 (maili mraba 380,000).
Mkuu wa kampuni ya Elon Musk amethibitisha kwamba kampuni hiyo itaunda betri hiyo katika kipindi cha siku 100, na ikishindwa kufanya hivyo basi itaunda betri hiyo bila malipo.
Betri hiyo itakuwa na uwezo wa megawati 100 (megawati 129 kwa saa), na inatarajiwa kuanza kutumiwa mwaka huu.
"Bila shaka kuna changamoto kadha, kwa sababu itakuwa betri kubwa zaidi duniani kwa mbali," Musk alisema akiwa Adelaide Ijumaa.
Aliongeza kuwa "betri inayoifuata hiyo kwa ukubwa ina uwezo wa megawati 30".
Betri hiyo mpya ya Tesla, ambao wameshirikiana na kampuni ya nishati ya upepo ya Neoen, itakuwa ikifanya kazi bila kuzimwa na itatoa umeme zaidi hasa wakati wa dharura.
"Itakabilisha kabisa jinsi kawi mbadala inavyohifadhiwa, na pia kuimarisha mfumo wa kusambaza umeme wa jimbo la Australia Kusini Weatherill alisema.
Siku 100 alizoahidi Musk zitaanza kuhesabbiwa baada ya mkataba kutiwa saini rasmi.

Tesla wamekuwa wakipanua biashara yao ya uundaji wa betri sawa na uundaji wa magari ya umeme.

Related Posts:

  • UNAWEZA KUSAFIRI UKITUMIA NDEGE ISIYO NA RUBANI....? Hilo ndilo swali mamilioni ya watu huenda wakajiuliza siku za usoni ikiwa wanataka kusafiri kwenda likizo kote duniani. Tunaposogea karibu na kutumia magari yasiyokuwa na dereva, ambayo tayari yameingia barabarani katika… Read More
  • CHINA KUZINDUA MTANDAO USIODUKULIWA…. Wakati udukuzi wa mitandao wanapoendesha udukuzi zaidi, China inatarajiwa kuzindua mtandao usiodukuliwa ikimaanisha kuwa itakuwa rahis kugundua kabla ya wadukuzi kuingia. Mradi huo wa kichina katika mji wa Jinan na unau… Read More
  • BETRI KUBWA ZAIDI DUNIANI KUUNDWA.. Betri kubwa zaidi ya lithium duniani itaundwa na kuwekwa nchini Australia, kupitia makubaliano kati ya kampuni inayounda magari ya kutumia umeme ya Tesla na kampuni ya kawi ya Australia Neoen. Betri hiyo inatarajiwa kul… Read More
  • SAMSUNG YATUMIA SEHEMU ZA NOTE 7 KUUNDA SIMU MPYA….. Kampuni ya mawasiliano ya Samsung imeanza kuuza simu nyingine ambazo inasema imetumia baadhi ya sehemu na vipande vilivyokuwa kwenye simu za Galaxy Note 7 ambazo zilikumbwa na matatizo. Simu hizo za Galaxy Note 7 ziliku… Read More
  • TCRA YATOA ONYO KUHUSU VIRUSI MTANDAONI… Kufuatia tishio la kuwapo programu mtumishi (software) yenye virusi aina ya WannaCry, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kwa watumiaji wa kompyuta kutofungua viambatanishi wasivyovijua kwenye barua pepe za… Read More

0 comments:

Post a Comment