Watu
16 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya ndege ya jeshi la Marekani waliyokuwa
wakisafiri nayo kuanguka kusini mwa jimbo la Mississippi, Jumatatu jioni.
Ndege
hiyo ilianguka na kushika moto katika eneo la LeFlore, umbali wa kilometa 160
kutoka katika jiji la Jackson.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa idara ya dharura ya ya Leflore, Fred Randle abiria wote
walikuwa wanajeshi na hakuna hata mmoja aliyesalimika ndani ya ndege hiyo.
Gavana
wa jimbo la Mississippi, Phil Bryant amesema kuwa tukio hilo ni janga kubwa
kwani askari hao walikuwa kazini wakijitolea maisha yao kila siku kuhakikisha
wananchi wanafaidi uhuru wao kwa amani.
“Watu wetu wanaume na wanawake walikuwa kwenye
sare zao wakijitolea maisha yao kila siku kulinda uhuru wetu,” alisema Gavana
Bryant.
Bado
hakuna maelezo rasmi ya kina kutoka kwa vyombo vya usalama kuhusu tukio hilo la
kuanguka kwa ndege ya jeshi ikiwa ni pamoja na chanzo cha ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment