Thursday 6 July 2017

SIRRO: DAWA YA MOTO NI MOTO………

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro,amesema wanaotekeleza mauaji dhidi ya raia katika eneo la Kibiti mkoani Pwani wametumwa vibaya, na wao watapelekwa vibaya vibaya.

Sirro alisema hayo jana Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa magari manne na Kampuni ya Great Wall Motor and Haval Company kutoka nchini China yatakayotumiwa na jeshi hilo.
“Tatizo la mauaji ya raia huko Kibiti na maeneo mengine nchini, nataka kusema si kawaida yangu kuongea sana, ila sio muda mrefu yatakwisha, hadi sasa tunakwenda vizuri na wale ambao wametumwa kutekeleza mauaji hayo wataona majibu yake,” alisema Sirro.
Pia aliwataka viongozi wa vijiji na Serikali za mitaa nchini kote kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kukabiliana na wimbi la uhalifu.
 Tangu wahalifu kuanza kutekeleza mauaji kwenye maeneo ya Kibiti na Mkuranga mkoani Pwani, zaidi ya watu 30 wamefariki dunia wakiwamo askari polisi zaidi ya 10, viongozi wa Serikali za vijiji na kata.

 Jeshi la Polisi limekuwa likiendesha operesheni maalumu kwenye eneo hilo na mara kadhaa limetangaza kupambana na wahalifu hao na kufanikiwa kuua baadhi yao

0 comments:

Post a Comment