![]() |
Winston Blackmore afika mahakamani huko Cranbrook |
Viongozi wawili wa dini nchini Canada
wamepatikana na hatia ya kuoa wake wengi.
Mahakama iliambiwa kuwa Winston Blackmore mwenye umri wa miak 61
alioa wanawake 24, naye mwanamume ambaye alikuwa ni mkwe wake James Oler akaoa
wanawake 5.
Wote walipatikana na hatia ya shtaka moja la kuwaoa wanawake
wengi na kila mmoja anakabiliawa na kifungo cha miaka mitano jela.
Hukumu hiyo imetajwa
kuwa mtihani mkubwa kwa uhuru wa kidini nchini Canada.
Blackmore na Oler ni kutokna jamii moja ya dini ya karibu watu
1500 ambayo ilianzishwa mwaka 1946.
![]() |
James Oler akifika kotini |
Wote hao walikuwa ni
makasisi wa dhehebu lililojitenga kutoka kanisa la Fundamentalist Church of
Jesus Christ of Latter-Day Saints (FLDS)
Bwana Blackmore alifukuzwa kutoka FLDS mwaka 2002 na mahala pake
pakachukuliwa na bwana Oler.
Matawi ya dhehebu
hilo yako nchini Marekani ambapo kuna wanachama karibu 10,000
Kuoa wanawake wengi ni haramu chini ya sheria za Canada, Palisi
nchini Canada walianza kuchunguza dhehebu hilo mnamo miaka ya 1990.
![]() |
Winston Blackmore mwaka 2008, inakisiwa ana watoto 145 |
0 comments:
Post a Comment