Wednesday, 12 July 2017

PAPA FRANCIS ATOA UTARATIBU MPYA WA KUWATANGAZA WATAKATIFU….

Baba mtakatifu papa Francis, ameongeza vigezo na utaratibu wa kuwatangaza watakatifu katika kanisa katoliki, katika kile kinachoonekana kama mabadiliko makubwa kufanywa katika kanisa hilo baada ya karne nyingi zilizopita.

Katika barua iliyotolewa na kanisa hilo mjini Vatican imeeleza juu ya hatua zitakazoashiria utakatifu ni pamoja na kitendo cha kuacha maisha ya mtu ili kuokoa wengine Kama kitendo cha tofauti na kuuawa, kuelekea njia ya utakatifu.
Tabia ya kujia maisha yako hadi kufa kama njia ya kutekeleza sheria za kikristo, na kwamba kingeweza kukubaliwa na wakatoliki na inaweza kutumika kwa Wakatoliki ambao kwa hiari walichukua nafasi ya Wayahudi waliotakiwa kuuawa katika kambi za kifo za Nazi, kwa mfano.
Hali hiyo inaingia katika kipengele cha nne katika hatua za kutangazwa kwa watakatifu.
Baada ya kufariki, uzuri wa Kikristo wa kipekee na sifa ya ukamilifu baada ya kifo ni kutangazwa mtakatifu ama mwenye heri.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment