Thursday, 6 July 2017

KABURI LA MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA UGANDA LAFUKULIWA…

Kaburi la Mtunzi wa Wimbo wa Taifa wa Uganda marehemu George Kakoma limefukuliwa na watu wasio julikana, huku kukiwa na wasiwasi kwamba mabaki ya mwili wake yameibiwa.

Gazeti la Daily Monitor la Uganda, limechapisha picha ya kile kilichoonekana kuchimbuliwa kaburi hilo na kuharibiwa.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, polisi wa eneo hilo na mjane wa marehemu wameomba kibali mahakamani kuweza kuchimbua kaburi hilo, ili kuweza kuthibitisha kama mabaki yake yapo ama yameondolewa.

Marehemu Kakoma alifariki dunia miaka mitano iliyopita.

Related Posts:

  • KASHMIR:MARUFUKU MATUMIZI YA ANASA….. Serikali ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa. Wazazi wa bibi harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, au mia nne ikiwa mtoto wa kiume atakuwa anaoa. Idadi ya aina … Read More
  • MUGABE ANAWEZA KUPIGIWA KURA AKIWA MAITI.. Grace Mugabe na mumewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti. Bwana Mugabe, ambaye ataku… Read More
  • SIMU YA ADOLF HITLER KUPIGWA MNADA MAREKANI. Simu iliokuwa ikitumiwa na kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler kupigwa mnada Marekan Simu iliyokuwa ikitumiwa na Adolf Hitler wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia itapigwa mnada nchini Marekani mwisho mwa juma hili. Simu… Read More
  • WABUNGE WAIDHINISHA KILIMO CHA BANGI UHOLANZI. Bunge la chini nchini Uholanzi, limeidhinisha kuhalalishwa kwa kilimo cha bangi. Mswada huo ulioidhinishwa utawakinga wakulima wa bangi, ambao wanatimiza masharti fulani dhidi ya kuadhibiwa. Mswada huo bado haujaidhini… Read More
  • NJAA YASABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU 100 SOMALIA... Waziri mkuu wa Somalia Hassan ali Khaire, amesema watu mia moja na kumi wamefariki kutokana na visa vinavyo husiana na ukame na baa la njaa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo, katika kipindi cha saa nane zilizo… Read More

0 comments:

Post a Comment