![]() |
Lindiwe Sisulu |
Chama kiku cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance (DA)
kimetaka kuelezwa na waziri wa nyumba Lindiwe Sisulu, jinsi idara yake ilitumia
dola 770,000 kwa maua na zawadi zingine wakati wa kipindi cha bajeti cha mwaka
2013/2014.
Utata unaibuka wakati
Bi Sisulu, binti wa mpinzani mkubwa wa utawala wa ubaguzi wa rangi Walter
Siusulu, anakabaliana na wapinzani wengine kuchukua nafasi ya Rais Jacob Zuma,
kama kiongozi wa chama tawala cha ANC.
Bi Sisulu alifichua
matumizi hayo akijibu swali la bunge, na sasa chama cha DA kinataka orodha yote
ya watu walionufaika kutokana na pesa hizo.
"Pesa hizo
zingetumiwa kujenga nyumba 100 za gharama ya nchini na kusaidia kukabiliana na
suala la ukosefu wa nyumba nchini Afrika Kusini," chama hicho kilisema.
Bi Sisulu hajazungumza
chochote kuhusu taarifa hiyo ya DA.
Siku ya Jumamosi
alitoa wito kwa wafuasi wake kufanya kampeni ya kuchaguliwa kwake kwa maadili
mema na kuapa kupambana na ufisadi.
Mshindi anatarajiwa
kuwa mgombea wa uara wa chama mwaka 2019.
0 comments:
Post a Comment