Monday, 13 November 2017

MAHAKAMA YAMHUKUMU LULU MIAKA 2 GEREZANI...

Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.


Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Baada ya hapo Jaji Rumanyika aliwapa nafasi upande wa mshtakiwa kujitetea ambapo wakili wake Peter Kibatala alimtetea mshakiwa kwa kusema kuwa mshtakiwa anategemewa na familia yake akiwemo mama yake na mama yake mdogo.

Baada ya hapo Jaji Rumanyika alitoa hukumu yake na kumuamuru mshtakiwa kwenda jela kwa miaka miwili.


Elizabeth Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Charles Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake, mnamo April 7, 2012

Reactions:

0 comments:

Post a Comment