Wanajeshi 18 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wamepandishwa
kizimbani kwa mara ya kwanza wakikabiliwa na kesi ya ubakaji wa halaiki wa
watoto.
Wanajeshi hao wanadaiwa kuwabaka watoto wa kike 46 katika kijiji cha
Kavumu, na kwamba kati yao walikuwemo wenye umri hadi miezi 18 tu.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya mwaka 2013 na 2016 kwa
sababu za imani ya kishirikina, kuwa damu ya wasichana bikira ingeweza kuwapa
nguvu ya ajabu na ulinzi.
Hata hivyo kiongozi wa wanajeshi hao anayetambulika kwa jina la
Frederic Batumike na wenzake, walikana mashtaka hayo.
Makundi ya haki za binadamu yanaamini ufunguzi wa kesi hizo, utamaliza
utamaduni wa ubakaji unaochukuliwa kama sehemu ya nguvu ya kivita nchini humo.
0 comments:
Post a Comment