Monday 13 November 2017

AUAWA KISA KUSAFIRISHA NG'OMBE….

Viongozi wa kijamii katika mji wa Rajasthan nchini India, wanasema mtu mmoja ambaye ni muislam ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoamini ng'ombe kuwa mungu wao.

Ummar Khan alikua akisafirisha ng'ombe yeye na mwenzake katika kitongoji cha Alwar wakati walipovamiwa na wahindu.
Wanasema kwamba mwili wa kijana huyo ulitupwa karibu na reli kuharibu ushahidi.
Polisi katika mji wa Rajasthan wameanzisha upelelezi juu ya tukio hilo.
Wahindu huamini kuwa ng'ombe ni mungu kwao, na huwachukulia kwa namna ya upekee sana.


Zaidi ya watu kumi wameuawa tokea mwaka 2015 kwa sababu kama hizo.

0 comments:

Post a Comment