Muuguzi mmoja
anayetumikia kifungo cha maisha jela kwa kuwauwa wagonjwa wawili kaskazini mwa
Ujerumani, sasa anashukiwa kuhusika na visa 84 vya mauaji.
Hayo yamesemwa na maafisa wa polisi nchini Ujerumani.
Muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 40, ametajwa kwa jina Niels
H, chini ya sheria za kuripoti habari nchini Ujerumani, alihukumiwa kwa kosa la
kujaribu kuuwa mnamo mwaka 2006 na kosa la mauwaji mwaka 2015.
Wahasiriwa wake walidungwa dawa yenye sumu, katika kitengo
cha matibabu alikokuwa akifanyia kazi.
Jamaa za wagonjwa waliofariki kwenye zahanati alikokuwa
akifanya kazi, wameomba polisi kuendeleza uchunguzi zaidi.
Tume maalum ilibuniwa mwaka 2014 kuchunguza ukubwa wa uhalifu
huo, ambao unaweza kumfanya kuwa muuwaji mkubwa zaidi nchini Ujerumani baada ya
mauwaji yaliyotokea kulipomalizika vita kuu vya kwanza na vya pili vya Dunia,
pamoja na ile ya enzi ya utawala wa Nazi.
Matibabu
aliyokuwa akiwapa wagonjwa, yalisababisha matatizo makubwa ya kuzima kwa moyo
au kushindwa kufanya kazi kwa mishipa ya damu na matatizo ya kupumua hatua
iliyomfanya mgonjwa kuanguka ghafla na kuzimia.
Baada ya mgonjwa kuonekana kama amefariki, anawapa dawa
nyingine ya kuwarejeshea uhai.
Majaji wanasema kuwa, alichochewa na hamu ya kupata umaarufu
na sifa kwa watu, kwa kuwarejeshea tena uhai wagonjwa aliokuwa amewapa dawa
hiyo ya sumu.
Wakati wa kesi iliyofanyika mwaka 2015, alikiri kuwapa zaidi
ya wagonjwa 90 dawa hiyo.
Polisi wanasema kuwa kasoro inarudi nyuma hadi mwaka 2,000
katika kliniki moja mjini Oldenburg.
Wanasema kuwa wafanyikazi walifanya mkutano mwaka 2001
kujadili viwango vya kushangaza vya vifo na na matendo ya kujaribu kufufua watu,
lakini hawakuripoti visa hivyo na badala yake Niels H alihamishiwa hadi
zahanati nyingine iliyoko Delmenhorst.
Tume maalum ya polisi ilibuniwa mnamo mwaka 2014 ili
kuchunguza kesi hiyo.
Ilichunguza mamia ya rekodi ya kimatibabu na kufukua jumla ya
maiti 134, ili kufanyia majaribio chembechembe ya dawa iliyotumika.
Uchunguzi huo aidha ulitatizwa pakubwa kwani baadhi ya maiti
ya wahasiriwa ilichomwa baada ya kufa.
"Matokeo haya aidha yanaendelea kutatiza uhalisia wa
fikra za watu," amesema mkuu wa polisi Oldenburg, Johann Kuhme. "sio
rahidi kusema ni watu wangapi waliuwawa."
Bwa Kuhme ameonya kuwa huenda idadi ya waliuwawa ikaongezeka.
Kuna uwezekano kuwa kesi mpya itawasilishwa mwanzo wa mwaka ujao wa 2018,
amesema.
0 comments:
Post a Comment