Wednesday, 16 August 2017

UBAKAJI WAITAFUNA UNGUJA..

Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, inakabiliwa na kasi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsi, ikiwemo matukio ya ubakaji na mimba kwa wanafunzi.


Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi, wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Kaskazini mbele ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein katika ziara ya kuangalia maendeleo ya mkoa huo.
Hata hivyo Mwinyi amesema kuwa, wameanza kudhibiti vitendo hivyo kwa kutoa elimu pamoja na kesi hizo kusikilizwa haraka haraka katika mahakama zilizopo katika mkoa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman alisema tayari vyombo vya sheria ikiwemo mahakama na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na jeshi la Polisi wamenza kuzipatia ufumbuzi wa haraka kesi za udhalilishaji wa kijinsia.

Related Posts:

  • WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI….. Waalimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu… Read More
  • WATOTO WAZUIWA KWENDA SHULE KUHOFIA KUPATA MIMBA Kutokana na tatizo la upungufu wa walimu katika Shule ya Msingi Mbalawala Manispaa ya Dodoma, wazazi wa watoto wanaosoma shuleni hapo wamewazuia watoto wao kwenda shule kuanzia leo hadi hapo watakapopelekewa walimu wa ku… Read More
  • NECTA YAZIDI KUWABANA WALIOGHUSHI VYETI Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine. Tangazo hi… Read More
  • WANAFUNZI KUFUNZWA KUHUSU NJIA ZA KUTOA TALAKA INDIA… Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu. Shule ya Dargh-E-Ala Hazrat inayodhibiti madrassa 15,000 za Kiislamu ilitangaza hilo kufuatia agizo… Read More
  • UBAKAJI WAITAFUNA UNGUJA.. Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, inakabiliwa na kasi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsi, ikiwemo matukio ya ubakaji na mimba kwa wanafunzi. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi, wa… Read More

0 comments:

Post a Comment